Katika mkoa wa Mbeya, Elimika Organization ilitekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa wakulima wa viazi ambao tayari walikuwa na uzoefu katika zao hili. Tofauti na Gairo ambako wakulima walihamishia mkazo kutoka parachichi kwenda viazi, wakulima wa Mbeya walikuwa tayari wakilima viazi lakini kwa kutumia mbinu za kitamadoni zenye tija ndogo. Mradi huu uliwapatia mafunzo ya hali ya juu kupitia wataalamu mbalimbali ili kuinua kiwango chao cha uzalishaji na kuwafanya washindane katika masoko makubwa. Agriterra waliwapa mafunzo ya biashara ya kilimo na utawala bora, HZPC waliwafundisha mbinu za kisasa za kilimo na umuhimu wa mbegu bora zilizoidhinishwa, na Mapinga Premium Foods waliowafundisha kuhusu mahitaji halisi ya soko na viwango vinavyotakiwa na wauzaji wakubwa. Mafunzo haya yamewasaidia wakulima wa Mbeya kubadilisha mawazo yao kutoka kwa kilimo cha kujikimu tu hadi kilimo cha kibiashara chenye faida, na kuwapa uelewa wa kina wa jinsi ya kuboresha ubora wa viazi zao ili kufikia viwango vya soko la kisasa.